CHINA-INTERPOL-HAKI-UFISADI

Rais wa shirika la Polisi wa Kimataifa ajiuzulu

Rais wa shirika la polisi wa kimataifa Meng Hongwei ametoweka tangu septemba 25,2018.
Rais wa shirika la polisi wa kimataifa Meng Hongwei ametoweka tangu septemba 25,2018. Jeff Pachoud/Pool via Reuters

Shirika la polisi wa kimataifa (Interpol) limetangaza kwamba rais wake Meng Hongwei amejuzulu kwenye wadhifa wake. Uamuzi huu unakuja saa chache kabla ya China kukiri kuwa inamshikiliwa Meng kwa madai ya ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

China imethibitisha kuwa inamshikilia Mkuu wa Polisi wa Kimataifa Interpol Meng Hongwei. Beijing inasema imechukua hatua hii kwa madai kuwa anakabiliwa na madai ya ufisadi na uchunguzi unaendelea.

Meng alitoweka baada ya kuondoka katika makao makuu ya Iterpol mjini Lyon nchini Ufaransa mwezi Septemba kwenda nchini China, lakini hakurejea kazini.

Shirika la polisi wa kimataifa Interpol linasema kuwa lina wasiwasi kuhusu hali ya sasa ya Rais wake.

Meng Hongwei alichaguliwa rais wa Interpol mwezi Novemba mwaka 2016.

Meng ni raia wa kwanza wa China kuchukua wadhifa huo na anatarajiwa kuwa katika wadhifa huo hadi mwaka 2020.

Kabla ya kuchukua wadhifa huo, Bw Meng alikuwa naibu waziri wa masuala ya usalama wa umma nchini China na bado yeye ni mwanachama wa cheo cha juu wa chama cha Communist.