CRIMEA-USALAMA

Kumi na nane wauawa katika shambulizi dhidi ya Chuo cha kiufundi Crimea

Mbele ya chuo cah kiudundi cha Kerch, Crimea, ambako mlipuko ulisababishwa vifo watu 18, hii 17 Oktoba 2018
Mbele ya chuo cah kiudundi cha Kerch, Crimea, ambako mlipuko ulisababishwa vifo watu 18, hii 17 Oktoba 2018 RFI/Capture d'écran

Takriban watu 18 wameuawa na 50 kujeruhiwa katika mlipuko unaotajwa kuwa wa "kigaidi" katika Chuo cha kiufundi huko Kerch Crimea. Shambulio hilo limetokea Jumatano hii Oktoba 17.

Matangazo ya kibiashara

Crimea ni eneo lililounganishwa na Urusi kutoka Ukraine mnamo mwaka 2014.

Kifaa cha kulipuka kiliyojaa vitu vya chuma kililipuka katika mgahawa wa shule mapema asubuhi. Wengi wa waathirika ni vijana. Kwa mujibu wa wachunguzi, huku wakibaini kwamba wanafunzi wengi waliuawa kwa kupigwa risasi.

Mkuu wa shule, Olga Grebennikova, alikuwa akiondoka shuleni wakati tukio hilo lililpotokea.

"Wamemuua mdogo wangu Nastia, na walimuua kwa kumpiga risasi mama yake," Olga Grebennikova amesema kwenye televisheni ya mdandaoni ya KerchNetTV. Maiti zipo kila mahali, ikiwa ni pamoja na miili ya watoto. Hili ni shambulio la kigaidi, kama lile lilotokea Beslan. Waliingia shuleni dakika 5 hadi 10 baada ya mimi kuondoka. Walilipua bomu ndani ya ukumbi, vio vya madirisha yote vimevunjika. "

Kwa mujibu wa msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, bado wanashikilia hoja ya kuwa huenda shambulio hilo limekuwa la kigaidi na Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa rambirambi zakkwa ndugu wa waathirika.