URUSI-MAREKANI-TRUMP-NYUKLIA

Gorbachev aionya Marekani dhidi ya kujitoa kwenye mkataba wa INF

Kiongozi wa mwisho wa USSR (Urusi ya zamani) Mikhail Gorbachev, hapa ilikuwa mwezi Novemba 2014. Alitia saini makubaliano kuhusu nyuklia na Rais wa Marekani Donald Reagan.
Kiongozi wa mwisho wa USSR (Urusi ya zamani) Mikhail Gorbachev, hapa ilikuwa mwezi Novemba 2014. Alitia saini makubaliano kuhusu nyuklia na Rais wa Marekani Donald Reagan. AFP PHOTO / ODD ANDERSEN

Mikhail Gorbachev, kiongozi wa zamani wa Urusi, ameionya Marekani kutothubutu kujitoa kwenye mkataba uliotiliwa saini kati ya Urusi na nchi hiyo. Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump alisema ataiondoa nchi yake katika mkataba wa nyuklia waliotiliana saini na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Mikhail Gorbachec amemtaja Trump kama "mtu asiye kuwa na busara".

 

Hata hivyo baadhi ya wabunge wa chama cha Republican nchini Marekani, wametangaza kuunga mkono uamuzi wa rais Donald Trump, ambaye amesema ataiondoa nchi yake katika mkataba wa nyuklia waliotiliana saini na Urusi.

Mnamo mwaka 1987, Urusi na Marekani zilitiliana saini mkataba huu kumaliza vita baridi huku kila nchi ikiridhia kuachana na utengenezaji wa silaha za nyuklia, lakini sasa rais Trump anasema Urusi imekiuka makubaliano hayo.

Serikali ya Urusi imeionya Marekani dhidi ya uamuzi wake ambao imesema ni hatari kwa usalama wa dunia hasa wakati huu dunia ikiwa katika kipindi cha kupinga matumizi na utengenezaji wa silaha za maangamizi.

Katika miezi ya hivi karibuni Marekani na Urusi ziliingia katika mvutano mkubwa, uliosababisha hata pande mbili hizo kuchukua hatua za kufukuziana maafisa wao wa kibalozi.

Wakati huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonia Guterres alisema hofu yake ni kwamba mwelekeo wa mvutano huo unafanana kidogo na zama za vita baridi kati ya Marekani na Urusi lakini wakazi wa zama hizo pande mbili hizo zilikuwa na udhibiti wa mvutano huo.