Mvutano wa kisiasa waendelea Sri Lanka
Imechapishwa:
Rais wa Sri Lanka na Spika wa bunge, wameshindwa kutatua mvutano wa kisiasa nchini humo, baada ya kufutwa kazi kwa Waziti Mkuu. Wadadisi wanasema juhudi za amani zinazidi kuwa hatarini nchini Sri Lanka.
Rais Maithripala Sirisena hadi sasa hajaamua kuitisha vikao vya bunge, kutatua suala hili baada ya kumfuta kazi Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe.
Uamuzi huo wa rais, umekatiliwa vikali na Mwanasheria Mkuu ambaye amaesema rais hana mamlaka.
Mapema wiki hii Sipka wa Bunge la Sri Lanka, Karu Jayasuriya alionya kuwa mgogoro wa kisiasa unaonendelea nchini humo unaweza kusababisha “umwagikaji damu”, huku akitaka wabunge waruhusiwe kutatua mvutano kati ya Rais na Waziri Mkuu aliyeondolewa Ranil Wickremesinghe.
Rais alimteua kiongozi wa zamani aliyekuwa na nguvu kubwa Mahinda Rajapakse kuwa Waziri Mkuu, na hivyo kuiacha nchi hiyo kuwa na watu wawili wanaodai wana mamlaka ya kuendesha serikali.