JAPAN-NISSAN-MITSUBISHI-UCHUMI

Uhusiano kati ya Ufaransa na Japani matatani kufuatia kukamatwa kwa Carlos Ghosn

Carlos Ghosn, Mwenyekiti wa kampuni za kutengeneza magari za Renault-Nissan, Oktoba 1, 2018.
Carlos Ghosn, Mwenyekiti wa kampuni za kutengeneza magari za Renault-Nissan, Oktoba 1, 2018. REUTERS/Denis Balibouse

Hisa za kampuni za kutengeneza magari nchini Japan Nissan na Mitsubishi, zimeshuka baada kukamatwa kwa Mwenyekiti Carlos Ghosn kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha. Bw Ghosn pia ni Kiongozi Mkuu wa kampuni ya kutengeneza magari nchini Ufaransa ya Renault.

Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa kwa Ghosn kumetikisa masoko ya biashara ya kampuni hizo ambazo zinatengeza magari ya kuyauza duniani, hali ambayo pia imeathiri biashara katika masoko ya Tokyo.

Kufuatia hali hiyo pia hisa za Renault nchini Ufaransa zimeshuka 7% tangu Jumatatu wiki hii.

Kwa sasa makampuni ya Renault/NIssan/Mitsubishi inachukuwa nafasi ya kwanza mbele ya kampuni ya Toyota.

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hizo watakutana siku ya Alhamisi na kufikia uamuzi wa kumfuta kazi Bwana Ghosn ambaye sifa yake nzuri katika kampuni hiyo sasa, imepakwa tope kutokana na madai yanayomkabili.

Licha ya kukamatwa kwake, viongozi wa mashtaka nchini Japan hawajaeleza kwa kina kuhusu kukamatwa kwake, lakini ripoti zilizochapishwa kwenye Magazeti nchini humo zinaeleza kuwa, Ghosn alitumia vibaya zaidi ya Yen Bilioni tano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.