UFARANSA-JAPANI-GHOSN-UCHUMI

Kesi ya Carlos Ghosn: Kampuni ya Nissan yachunguzwa na vyombo vya sheria vya Japan

Nissan inahusika kwa kuficha mshahara halisi wa mwenyekiti wake wa bodi ya wakurugenzi Carlos Ghosn, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Japan.
Nissan inahusika kwa kuficha mshahara halisi wa mwenyekiti wake wa bodi ya wakurugenzi Carlos Ghosn, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Japan. REUTERS/Issei Kato/File Photo

Kampuni ya kutengeneza magari ya Nissan, kama taasisi ya kisheria, inachunguzwa na vyombo vya sheria vya Japan kufuatia kukamatwa kwa mwenyekiti wake wa bodi ya wakurugenzi Carlos Ghosn siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na gazeti la Asahi, kampuni ya Nissan inaweza kushtakiwa kwa kutoa nyaraka zisizo sahihi za fedha kwa mamlaka ya kodi nchini Japan.

Vyombo vya habari vya Japani vinaendelea kufichua madai ya kukwepa kodi na ubadhirifu unaodaiwa kufanywa na Carlos Ghosn na mshirika wake wa karibu Greg Kelly, ambaye pia anashikiliwa, kwa ushirikiano na viongozi wengine wa kampuni hiyo ya Japan. Wakati huo huo shirika la Habari la Kyodo limetangaza kwamba Carlos Ghosn ataendelea kuzuiliwa kwa muda wa siku kumi.

Kulingana na uchunguzi wa ndani wa Nissan, Carlos Ghosn ameificha mamlaka ya kodi ya Japan na wanahisa wa Nissan nusu ya mapato yake, yenye thamani ya euro milioni 39, kati ya mwaka 2010 na 2015. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, pia alishindwa kuripoti kwa Mamlaka ya Masoko na Fedha kuhusiana na mabadiliko ya bei ya hisa ya Nissan, mwandishi wetu mjini Tokyo, Frederic Charles amearifu.

Nissan ilinahusika kwa kuficha mshahara halisi wa mwenyekii wake wa bodi ya wakurugenzi. Carlos Ghosn hakughushi data peke yake: kampuni pia inahusika, kwa hiyo Nissan inakabiliwa na mashitaka.

Kwa mujibu wa gazeti la Nikkei, maofisa wawili wa Nissan, walio karibu na Carlos Ghosn, walihusika katika kampuni tanzu ya Uholanzi kwa kununua nyumba za kifahari katika nchi nne na kumkabidhi Carlos Ghosn. Maofisa hao wawili wa Nissan wanashirikiana na mahakama baada ya kukubaliwa kupunguziwa hukumu ikiwa watahukumiwa.

Thierry Bolloré akaimu kwenye nafasi ya Carlos Ghosn

Bodi ya wakurugenzi ya Nissan inatarajiwa kuchukuwa uamuzi Alhamisi wiki hii wa kumumfuta kazi au la mwenyekiti wake. Na Mitsubishi Motors (MMC), pia mwanachama wa muungano huo, itakutana ili kuamua hatima ya Carlos Ghosn. Kwa upande wa Ufaransa, bodi ya wakurugenzi ya Renault, siku ya Jumanne jioni ilimteua namba mbili wa kampuni hiyo, Thierry Bolloré, kuchukua nafasi ya Carlos Ghosn, ambaye anaendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo. Bw Bolloré, mshirika wa karibu wa Carlos Ghosn tangu mwezi Februari mwaka huu, aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo kwenye kampuni ya Renault.