PAKISTAN-UGAIDI-CHINA

Pakistan: Watu wanne wauawa baada ya kushambuliwa kwa ubalozi mdogo wa China

Eneo la Ubalozi mdogo wa China ulioshambuliwa nchini Pakistan Novemba 23 2018
Eneo la Ubalozi mdogo wa China ulioshambuliwa nchini Pakistan Novemba 23 2018 REUTERS/Akhtar Soomro

Watu wenye silaha, wamewauwa watu wanne, baada ya kushambulia Ubalozi mdogo wa China mjini Karachi nchini Pakistan.

Matangazo ya kibiashara

Milio ya risasi ilisikika Ijumaa asubuhi nje ya Ubalizi huo mdogo katika eneo la Clifton.

Ripoti zinasema kuwa, polisi wamewauwa wavamizi hao kwa kuwapiga risasi.

Watu wenye silaha wanaosema wanapinga kuwepo kwa  miradi ya China Magharibi mwa Pakistan, wamedai kuhusika.

Katika tukio lingine, watu wengine 25 wameauwa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo , katika eneo la kuabudu.

Mara kwa mara Waislamu wa Kishia ambao ni wachache wamekuwa wakilengwa na wapiganaji wa Kisunni.