Mvutano waendelea kati ya Urusi na Ukraine
Imechapishwa:
Rais wa urusi Vladimir Putin amesema walinda mpaka wake walikuwa wakitimiza majukumu yao ya kijeshi walipodhibiti meli tatu za Ukraine katika pwani ya Crimea juma lililopita.
Hayo yanajiri wakati huu raisi wa ukraine akiwa tayari ametia saini sheria mpya ya kijeshi katika mipaka yake hatua inayozua mvutano zaidi kati yamataifa hayo mawili.
Kufuatia hali hiyo Nae Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuahirisha mazungumzo kati yake na raisi wa urusi Vladimir Putin.
Mkutano huo ulikuja baada ya Urusi kushikilia meli za Ukraine katika eneo la Kerch, eneo ambalo linaloingiliana na Bahari ya Azov.
Mapema wiki hii "kikao cha dharura" cha Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) na Ukraine kilifanyika mjini Brussels kwa ombi la Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg.