CHINA-MAREKANI-BIASHARA-UCHUMI

Biashara: China kutekeleza hatua ilizoafikiana na Marekani

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump wakutana uso kwa uso Desemba 1, 2018 Buenos Aires.
Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump wakutana uso kwa uso Desemba 1, 2018 Buenos Aires. REUTERS/Kevin Lamarque

China inatarajia kuanza kutekeleza hatua za biashara ilizoafikiana na Marekani wakati wa mkutano kati ya Marais Donald Trump na Xi Jinping, Wizara ya Biashara ya China imesema.

Matangazo ya kibiashara

"China itatekeleza mara moja makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili kwa bidhaa za kilimo, nishati, magari na bidhaa zingine," amesema msemaji wa wizara ya biashara ya China mbele ya vyombo vya habari, Gao Feng.

Taarifa hiyo inakuja siku tano baada ya mkutano kati ya Marais Donald Trump na Xi Jinping huko Buenos Aires, hatua ambayo huenda ikapunguza vita vya biashara kati ya nchi hizi mbili zinazostawi kiuchumi duniani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China tayari ilitangaza siku ya Jumatano "utekelezaji wa pointi maalum ambapo makubaliano yalifikiwa" katika wa mkutano huo kando ya mkutano wa G20, lakini bila maelezo zaidi. Gao Feng pia hakueleza ni hatua gani zitakazofuata.

Tangu Beijing na Washington kutangaza kwamba wamesitisha tofauti zao katika mgogoro wao mgumu wa kibiashara.