Pata taarifa kuu
INDONESIA-TSUNAMI-MAJANGA YA ASILI

Tsunami Indonesia: Idadi ya watu waliopoteza maisha yafikia 373

Pwani ya Carita katika Mkoa wa Banten Indonesia ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi na Tsunami "volkano" ya tarehe 22 Desemba 2018.
Pwani ya Carita katika Mkoa wa Banten Indonesia ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi na Tsunami "volkano" ya tarehe 22 Desemba 2018. Reuters/Adi Kurniawan
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Indonesia baada ya Tsunami kukumba miji ya pwani nchini nchini humo imefikia 373 na wengine wengi wamejeruhiwa. Waokoaji wanaendelea na zoezi la kutafuta watu wanaodaiwa kuwa wamekwama chini ya vifusi vya nyumba.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo wataalam wanaonya juu ya hatari ya kutokea kwa maafa makubwa yanayoweza kusababishwa na kulipuka kwa volkano ya Anak Krakatau.

Siku ya Jumamosi Tsunami ilipiga maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na eneo linalotenganisha visiwa vya Sumatra na Java.

Tsunami imesababisha watu 373 kupoteza maisha, zaidi ya elfu moja kujeruhiwa na 57 hawajulikani waliko, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu hii Desemba 24. Ripoti ya awali ibaini kwamba watu 222 ndio walipoteza maisha.

"Idadi ya waathirika itaendelea kuongezeka," amesema Sutopo Purwo Nugroho, msemaji wa Idara inayohusika na majanga.

Zoezi la kutafuta watu walio hai na miili ya watu waliopoteza maisha bado linaendelea.

"Jeshi na polisi wanashirikiana katika zoezi la uokoaji ili kuona kama watapatikana waathirika wengine," amesema Dody Ruswandi, afisa wa Idara inayohusika na majanga.

Zoezi la uokoaji linatarajiwa kuendelea kwa muda wa wiki moja, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Idara inayohusika na majanga

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.