UFILIPINO-HAKI

Rais Duterte adai kumyanyasa kimapenzi mjakazi wake

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, Septemba 15, 2018.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, Septemba 15, 2018. REUTERS/Erik De Castro

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameibua sintofahamu baada ya kutaja mara ngapi alimnyanyasa kimapenzi mjakazi wake. Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia taifa siku ya Jumamosi Desemba 29, 2018. Wakati huo huo mashirika ya haki za wanawake wametoa wito kwa Rais Rodrigo Duterte kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte imezua sintofahamu nchini humo na kuacha maswali mengi kuhusu hadi lini ataachana na ukatili wake?

Baada ya kujisifu kuwa aliua na kufanya vitendo vya ubakaji, hatimaye rais Duterte amesema kuwa wakati wa ujana wake, alimnyanyasa kingono mjakazi wake alipokuwa usingizini.

Rais Duterte ameshambuliwa kwa maneno makali Kanisa Katoliki, akimshutumu padri ambaye alikiri mbele yake kuhusu kitendo hicho kuwa na yeye pia alimnyanyasa kimapenzi mjakazi wake.

Kama ilivyokuwa kawaida, msemaji wa ofisi ya rais amesisitiza, akisema alichokisem arais Duterte ni kama tahadhari kwa unyanyasaji wa kingono unaoendelea katika taasisi mbalimbali za kanisa Katoliki.

Hata hivyo, licha ya kauli hiyo ya Rais Duterte, bado anaendelea kuungwa mkono katika kambi yake.