KOREA KASKAZINI-MAREKANI-NYUKLIA

Korea Kaskazini yaionya Marekani kuhusu mradi wake wa Nyuklia

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong KCNA via REUTERS

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un, amesisitiza kuwa ana nia ya dhati ya kuachana na mradi wa nyuklia, lakini anaonya kuwa hilo huenda litabadilika iwapo Marekani itaendelea kuiwekea vikwazo.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka, Kim Jong Un, imeacha njia panda diplomasia ya nchi yake pamoja na ile ya Marekani na Korea Kusini, iliyokuwa  imeanza kuimarika mwaka 2018.

Mwaka uliopita, rais wa Marekani Donald Trump alikutana na Kim Jong Un katika mazungumzo ya kihistoria kuhusu nyuklia lakini, hakuna matokeo makubwa ambayo yameshuhudiwa hadi sasa.

Kiongozi huyo wa Korea Kasakzini katika hotuba yake amesisitiza kuwa iwapo Marekani haitatekeleza ahadi iliyotoa mbele ya dunia nzima, na kuondoa vikwazo vya kiuchumi  na kuacha shinikizo, huenda Pyongyang ikaja na mbinu mpya za kujilinda na kutetea maslahi yake.

Hata hivyo, amesema kuwa ataendelea kukutana mara nyingi na rais Trump kuzungumzia suala hili tata.