UTURUKI-URUSI-USHIRIKIANO

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuzuru Urusi Jumatano

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao Kremlin, Moscow tarehe 10 Machi 2017.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao Kremlin, Moscow tarehe 10 Machi 2017. Sergei Ilnitsky / POOL / AFP

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, anatarajia kuanza ziara ya kikazi nchini Urusi Jumatano wiki hii. Ziara hii inakuja siku chache baada ya Marekani kutangaza kuwa itawaondoa askari wake nchini Syria. Ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi unaendelea kuimarika.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya ofisi ya rais, Rais Erdoğan atafanya ziara ya siku moja siku ya Jumatano nchini Urusi na katika ziara hiyo atakutana na rais wa Urusi Vladmir Putin.

Moja kati ya mambo yatakayojiri katika ziara hiyo ni pamoja na mkutano utaofanyika jijini Moscow baina ya wajumbe na mawaziri wa pande hizo mbili. Katika mkutano huo mambo mbalimbali ikiwemo hali ya Syria na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili yanatarajiwa kuwa ajenda kuu za mkutano huo.

Uturuki ni mshirika wa mkuu wa Urusi na nchi hizi mbili zinaendelea kushirikiana katika vita nchini Syria dhidi ya kundi la Islamic State.