BANGLADESH-USALAMA

Watu 70 waangamia katika mkasa wa moto Bangladesh

Mkasa wa moto umeua takribani watu 70 katika jengo la kale huko Dhaka, mji mkuu wa Bangladesh, afisa wa kikosi cha Zima moto amesema.

Watu 50 wamelazwa hospitalini, wengine wako katika hali mbaya.
Watu 50 wamelazwa hospitalini, wengine wako katika hali mbaya. REUTERS/Mohammad Ponir Hossain
Matangazo ya kibiashara

Shughuli ya uokoaji inaendelea kutafuta miili iliyounguzwa kwa moto katika jengo hilo la ghorofa nne na inawezekana kuwa idadi ya watu waliouawa inawezekana kuongezeka, afisa huyo ameongeza.

Moto ulianza siku ya Jumatano usiku katika jengo ambalo lilikuwa limehifadhi vifaa vya plastiki na bidhaa za kemikali, kwa mujibu wa maafisa wa Zima Moto.

Moto ulisambaa katika majengo mengine ya eneo hlo la kihistoria la Dhaka, ambapo baadhi ya ya maengo hayo yalijengwa miaka 300 iliyopita. Ilichukuwa zaidi ya saa tano ili moto huo kudhibitiwa.

Watu 50 wamelazwa hospitalini, wengine wako katika hali mbaya, Julfikar Rahman, mkurugenzi wa Kikosi cha Zima Moto na ulinzi wa raia, ameliambia shirika la Habari la Reuters.