BANGLADESH-USALAMA

Bangladesh yachunguza kisa cha jaribio la utekaji nyara wa ndege Dhaka

Ndege iliyokuwa ikielekea Dubai ambayo iliponea kutekwa nyara kwenye uwanja wa ndege wa Chittatong Februari 24, 2019 Bangladesh.
Ndege iliyokuwa ikielekea Dubai ambayo iliponea kutekwa nyara kwenye uwanja wa ndege wa Chittatong Februari 24, 2019 Bangladesh. © AFP

Mamlaka nchini Bangladesh inapitia upya taratibu za usalama katika viwanja vyake vya ndege baada ya mtu, mgonjwa wa akili kulingana na uchunguzi wa awali, kujaribu kuteka nyara ndege iliyokuwa ikielekea Dubai. Tukio hilo lilitokea Jumapili usiku katika uwanja wa ndege wa Chittagong.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi maalum vya Bangladesh viliingilia kati na kufaulu kuwakomboa abiria 148 na wafanyakazi wa ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ya shirika la ndege la Biman Bangladesh wakati wa operesheni katika uwanja wa ndege Chittagong (kusini), ambapo ndege kutoka mji mkuu Dhaka ilikuwa imetua kabla ya kuelekea katika Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE).

Mtuhumiwa, raia Bangladeshi mwenye umri wa miaka 25, ambaye alijeruhiwa wakati wa operesheni ya vikosi vya usalama, alifariki dunia muda mfupi baada ya kukamatwa kwake. Alikuwa amekata tiketi ya kwenda mkoani kutoka Dhaka kwenda Chittagong.

Mamlaka wanatafuta kuelewa jinsi kijana huyo aliweza kuingia katika ndege na silaha, silaha ambayo matokeo ya kwanza yanaonyesha kuwa ilikuwa ni ya bandia.

"Uchunguzi unaendelea," mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri wa anga, " Marshal Nayeem Hasan ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Haiwezekani kukiuka usalama (kwenye uwanja wa ndege) kwa sababu mfumo unaoundwa na ICAO", International Civil Aviation Organization. Taratibu za usalama zinakaguliwa na makampuni ya kigeni.

Abiria mmoja amewambia waandishi wa habari kwamba mtekaji nyara alifyatua risasi mbili dakika kumi baada ya ndege kuondoka katika uwanja wa ndege wa Dhaka. Lakini mamlaka imesema leo Jumatatukuwa bunduki aliyotumia ni ya bandia.

"Kwa mujibu wa wale ambao waliona inaweza kuwa ni bunduki bandia," Bw Hasan amesema.

Baada ya operesheni ya vikosi vay usalama, ndege giyo iliruhusiwa kuendelea na safari yake.