JAPAN-GHOSN-UCHUMI-HAKI

Mke wa Carlos Ghosn afikishwa mahakamani Tokyo

Mke wa Carlos Ghosn, aliyerejea Japan baada ya kuondoka nchini humo, amefikishwa mahakamani jijini Toyko, nchini Japan, ili aweze kusikilizwa kuhusu tuhuma mpya za ubadhirifu zinazomkabili mume wake, vyombo vya habari vya Japan vimeripoti.

Carlos Ghosn (kushoto) na mkewe Carole wakiondoka katika ofisi ya mwanasheria Junichiro Hironaka, 3 Aprili 2019, Tokyo
Carlos Ghosn (kushoto) na mkewe Carole wakiondoka katika ofisi ya mwanasheria Junichiro Hironaka, 3 Aprili 2019, Tokyo © AFP
Matangazo ya kibiashara

Magazeti ya Asahi na Nikkei yameripoti kuwa Carole Ghosn amewasili katika mahakama mapema Alhamisi hii mchana.

Anatarajiwa kuhojiwa kama shahidi katika sehemu ya mwisho ya kesi hiyo, ambayo ilisababisha Bw Ghosn kurejeshwa jela Aprili 4, karibu mwezi mmoja baaada ya kuachiliwa huru kwa dhamana.

Carlos Ghosn, mwenye umri wa miaka 65, anatuhumiwa na ofisi ya mashitaka kupitisha mlango wa nyuma fedha za kampuni ya magari ya Nissan kupitia msambazaji wa magari ya Japani nje ya nchi.

Kulingana na ripoti ya uchunguzi wa ndani wa Nissan, sehemu ya pesa hizo iliwekwa kwenye akaunti za kampuni inayoongozwa na Carole Ghosn, "Beauty Yachts", iliyosajiliwa katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza.

Fedha hizo zilitumiwa kununua mashua ya anasa, yenye thamani ya euro milioni 12, ijulikanayo kwa jina la "Shachou" (jina la "Shatcho" linamaanisha tajiri kwa Kijapan), chanzo kilo karibu na kesi hiyo kimesema.