MAREKANI-KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Trump na Moon wakubaliana kuendeleza vikwazo dhidi ya Pyongyang

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na mwenzake wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House, Aprili 11, 2019.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na mwenzake wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House, Aprili 11, 2019. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alimpokea mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in siku ya Alhamisi katika White House, ametangaza nia yake ya kufanyika mkutano mpya na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, akibaini kwamba hana mpango wa kuondoa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump na Moon Jae-in, ambao walizungumza katika ikulu ya White House baada ya chakula cha mchana, walijadili uwezekano wa kufanyika mkutano mpya kati ya viongozi wa Korea mbili kwa lengo la kufufua mazungumzo kati ya Washington na Pyongyang.

Tangu kushindwa kwa mkutano wa Hanoi mwishoni mwa mwezi Februari, majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yamesimama. Kabla ya ziara ya Moon jijini Washington, washauri wake walisitiza haja ya kuanzisha tena majadiliano hayo.

"Mkutano wa tatu (pamoja na Kim Jong-un) unaweza kufanyika. Tunakwenda hatua kwa hatua. sio mchakato wa haraka, sijawahi kusema kuwa jambo hilo litakuwa," Trump alisema.

Aliongeza kuwa "mambo mazuri" yalitokana na mazungumzo na Pyongyang, ingawa hakupata kile alichotaka katika mikutano yake miwili ya kihistoria na kiongozi wa Korea Kaskazini Juni 12 jijini Singapore, kisha Februari 27 na 28 jijini Hanoi.