KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini yafanyia majaribio silaha mpya

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akihudhuria jaribio la silaha mpya, Novemba 16, 2018.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akihudhuria jaribio la silaha mpya, Novemba 16, 2018. REUTERS

Korea Kaskazini inasema imefanyia majaribio silaha mpya, iliyoeleza ni silaha ya mwongozo iliyo na nguvu, likiwa ni jaribu la kwanza baada ya mazungumzo kati ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump kumalizika bila ya mwafaka wowote miezi kadhaa iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya kina haijatolewa kuhusu jaribio hili. Wadadisi wa mambo wanaona kuwa huenda hii sio ishara kuwa Korea Kaskazini inataka kurejelea majaribio ya silaha zake za masafa marefu, ambayo yamekuwa yakitishia usalama wa Marekani na washirika wake.

Mwezi Novemba, jaribio lingine kama hili lilifanyilka na ikaonekana ni ishara ya kuishinikiza Marekani.

Hakuna juhudi zozote zilizopigwa kati ya Korea Kaskazini na Marekani, baada ya Kim Jong Un kukutana na rais Donald Trump mwezi Februari nchini Vietnam na mazungumzo hayo kumalizika bila ya makubaliano yoyote.

Wiki iliyopota, Kim alisema Trump anahitaji fikra sahihi ili kuwezesha mazungumzo hayo kuedelea.

Marekani inataka korea Kaskazini kuharibu mitambo yake yote ya nyukulia, huku Korea Kaskazini ikitaka Marekani kuiondolea vikwazo.