URUSI-AJALI

Arobaini na mmoja wapoteza maisha katika ajali ya ndege Urusi

Ndege ya shirika la ndege la Urusi la Aeroflot ikiwaka moto kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo, Moscow.
Ndege ya shirika la ndege la Urusi la Aeroflot ikiwaka moto kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo, Moscow. The Investigative Committee of Russia/Handout via REUTERS

Kulingana na ripoti ya awali, watu wasiopungua 41 wamepoteza maisha baada ya ndege ya shirika la Urusi la Aeroflot kutua kwa dharura na kulipuka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilikuwa imeabiri watu 78. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Urusi, watoto wawili na mhudumu mmoja ni miongoni mwa waliofariki.

Watu Thelathini na saba wamenusurika kati ya watu 78 waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watano, wachunguzi wamwbaini.

Video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha ndege hiyo ikitua katikati ya moto mkubwa. Mara baada ya kutua, abiria waliokolewa, licha ya kuwa kuna wengi ambao walipoteza maisha.

Shirika la ndege laUrusi, Aeroflot, limesema ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa ndege "kutokana na sababu za kiufundi", lakini halikufafanua zaidi.

Baada ya kutuwa kwa dharurua katika uwanja huo wa ndege , injini za ndege hiyo ziliwaka moto katika njia kuu za ndege, Aeroflot imesema katika taarifa.

Aeroflot limechapisha orodha ya walionusurika mkasa huo (kirusi) ambao kufikia sasa wametambuliwa, likiongeza kwamba litaendelea kutoa taarifa kadri wanavyozipokea.

Serikali ya mkoa wa Murmansk imetangaza siku tatu za maombolezo.