Waandishi wa habari wawili wa Reuters wapewa msamaha na kuachiliwa huru Burma
Waandishi wa habari wawili wa shirika la habari la Reuters walikuwa wakizuiliwa jela nchini Burma baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba mnamo mwezi Septemba mwaka jana kwa kuvujisha siri za serikali wamesamehewa na kuachiliwa huru leo Jumanne (Mei 7) na mamlaka ya Burma, mashahidi wamesema.
Imechapishwa:
Wa Lone, 33, na Kyaw Soe Oo, 29, wametoka jela la Insein nje ya mji wa Yangon, wamesema. Waandishi wa habari wawili wa wa Reuters, raia wa burma walikuwa kizuizini kwa siku zaidi ya 500 baada ya kukamatwa mwezi Desemba 2017 wakati walikuwa wakichunguza mauaji ya watu kumi kutoka jamii ya Rohingya wakati wa operesheni ya kijeshi Magharibi mwa Burma.
Hatua hii ya kuachiliwa huru inakuja baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba kwa kuvujisha siri ya serikali. hukumu ambayo ilithibitishwa mara mbili katika ngazi ya rufaa, hususan na Mahakama Kuu ya Burma - na baadaye waangalizi wengi walitaja kesi hiyo kuwa ni ya "ujanja".
Wakati kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa mahakamani, afisa wa polisi alikiri kuwa aliwatega waandishi wa habari wawili, kwa kuwakabidhi hati za siri wakati wa uchunguzi wao, kabla ya kukamatwa. Kukamatwa kwao kulitoa ushahidi wa vitisho dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Burma.
Wa Lone na Kyaw Soe Oo ni miongoni mwa wafungwa zaidi ya 6,500 walioachiliwa huru leo Jumanne.
Wadadisi wanasema huenda Burma ilitaka ipunguzi shinikio la kimataifa iliyokuwa ikikabiliana nalo.
Tangu kukamatwa kwao, Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa kwa mara kadhaa walitoa wito kwa kiongozi Aung San Suu Kyi, kuachilia huru waandishi hao wa habari, bila mafanikio. Burma bado inawazuia wafungwa 48 wa kisiasa.