KOREA KASKAZINI-MAREKANI- KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Korea Kaskazini: Makombora mapya mawili yarushwa kwenye Bahari ya Japani

Mvutano umeendelea kuongezeka kwenye rasi ya Korea. Korea Kaskazini imefanya uzinduzi wa makombora mapya mawili ya masafa mafupi Alhamisi hii, Mei 9, alasiri.

Korea ya Kaskazini tayari imrusha makombora katika Bahari ya Japan Jumamosi, Mei 4 (picha ya kumbukumbu).
Korea ya Kaskazini tayari imrusha makombora katika Bahari ya Japan Jumamosi, Mei 4 (picha ya kumbukumbu). Korean Central News Agency (KCNA)
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja siku tano tu baada ya mfululizo wa vifaa vya kulipuka kurushwa Jumamosi, Mei 4, kwenye Bahari ya Japani.

Utawala wa Kim Jong-un unaonekana kuwa unajaribu kuweka shinikizo kwa Marekani na Korea Kusini, wakati mazungumzo ya nyuklia yamesimama. Makombora haya mawili ya masafa mafupi yamerushwa kutoka kambi ya Sino-ri, kilomita 77 kaskazini magharibi mwa Pyongyang, jeshi la Korea Kusini limesema.

Makombora hayo yaliyorushwa kuelekea mashariki mwa nchi, moja lilikwenda umbali wa kilomita 420 na nyingine kilomita 270 yakiwa hewani,kwenye anga ya Korea Kaskazini, kabla ya kuanguka katika Bahari ya Japan.

Makombora haya yamerushwa wakati mjumbe maalum wa masuala ya nyuklia wa Marekani, Stephen Biegun, amewasili Alhamisi hii jijini Seoul kwa mazungumzo. "Korea Kaskazini imetaka kuonyesha Marekani kwamba suala haliko upande wao," mchambuzi Andrey Lankov kutoka Seoul amesema.

Ameongeza kuwa utawala "utaendelea kukumbusha kuwa ikiwa mkataba kuhusu vikwazo hautopatikana, basi inaweza kusababisha hali ya sintofahamu katika ukanda huo".

Urushaji huo wa makombora unakuja wakati Korea Kusini ina mpango wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa raia wa Korea Kaskazini, wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.