INDIA-MODI0-SIASA

Narendra Modi ashinda Uchaguzi Mkuu nchini India

Waziri Mkuu wa India  Narendra Modi amepata ushindi mkubwa baada ya chama chake cha Bharatiya Janata kushinda zaidi ya viti 300 kati ya 543 vya ubunge, vilivyokuwa vinawaniwa katika Uchaguzi Mkuu uliochukua mwezi mmoja.

Waziri Mkuu Narendra Modi akisherehekea baada ya ushindi wa Uchaguzi wa wabunge May 23 2019
Waziri Mkuu Narendra Modi akisherehekea baada ya ushindi wa Uchaguzi wa wabunge May 23 2019 REUTERS/Anushree Fadnavis
Matangazo ya kibiashara

Modi ametembelea makao makuu ya chama chake kusherehekea ushindi huu katika taifa hilo lenye demokrasia kubwa duniani baada ya wapiga kura Milioni 600 kushiriki katika Uchaguzi huo kwa kipindi cha wiki sita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri Mkuu Mondi amewashukuru raia wa nchi hiyo kwa kumrejesha madarakani kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano, na kuahidi kuwa imempa nguvu ya kufanya bidii zaidi.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa, Modi ana kazi kubwa kuliunganisha taifa hilo ambalo kuelekea Uchaguzi Mkuu, lilikuwa limegawanyika.

Tayari chama kikuu cha upinzani cha Congress, kinachoongozwa na Rahul Gandhi kimekubali kushindwa.