JAPAN

Watu 2 wauawa katika shambulio la kisu Japan

Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha nchini Japan, baada ya kushambuliwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa kisu nje kidogo ya mji mkuu wa Tokyo.

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe. AFP PHOTO/Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Polisi inasema mtoto wa shule mwenye umri wa miaka 12 na mwanaume mmoja ni miongoni mwa waliopoteza maisha mshambuliaji akiwajeruhi mamia ya watu wakiwemo watoto 7.

Shambulio hili lililotekelezwa kwenye mji wa Kawasaki kusini mwa mji mkuu wa Japan, ni tukio ambalo si la kawaida katika taifa hilo ambalo halina rekodi mbaya za uhalifu.

Polisi tayari wameanzisha uchunguzi kubaini sababu za mtu huyo kuwashambuliwa watu wazima pamoja na wanafunzi.

Kiyoshi Matsuda, kaimu mkurugenzi wa hospitali moja ambayo inatoa matibu kwa majeruhi, amewaambia waandishi wa habari kuwa mtoto wa miaka 12 na mtu mwenye umri wa miaka 39 wamepoteza maisha.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa mshambuliaji anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 50 ambapo nae alipoteza maisha kutokana na majeraha baada ya kujichoma kisu.

Vyombo vya huduma ya kwanza vinasema watu 16 walijeruhiwa katika tukio hilo.

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ametuma salama za pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na wale waliojeruhiwa, akilaani tukio hilo alilosema halikubaliki nchini mwake.