Pata taarifa kuu
HONG KONG

Hong Kong: Ofisi za Serikali zafungwa kutokana na maandamano

Waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wakiwa tayari kukabiliana na polisi
Waandamanaji kwenye mji wa Hong Kong wakiwa tayari kukabiliana na polisi 路透社。

Kiongozi wa jiji la Hong Kong Carrie Lam amewakosoa waandaaji wa maandamano kupinga sheria tata ambayo ingeruhusu ubadilishanaji wa wahalifu na China, akiyaita maandamano hayo “vurugu za kupanga".

Matangazo ya kibiashara

Lam amesema makabiliano kati ya waandamanaji na polisi hayakubaliki katika jamii iliyostaarabika.

Watu 72 ambao wana umri wa kati ya miaka 15 hadi 66 walijeruhiwa katika vurugu hizo, wakiwemo wanaume wawili ambao hali zao ni mbaya.

Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema wahalifu wanaoshikiliwa China wamekuwa wakiteswa na kulazimishwa kukubali makosa.

Wakosoaji wanahofia pia huenda sheria hiyo ikatumika kuwalenga wanasiasa wa upinzani ambao ni wakosoaji wa Serikali ya Beijing.

Wanasiasa wanaomuunga mkono Lam wanaunga mkono sheria hii ambayo pia utawala wa China umeikubali.

Serikali ya Hong Kong kwa upande wake imesema utekelezaji wa sheria hiyo utazingatia utu, haki na utawala wa sheria.

Bunge limeahirisha muswada wa sheria hiyo kusomwa mara ya pili ingawa inatakiwa kupigiwa kura Juni 20.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.