Pata taarifa kuu
CHINA-KOREA KASKAZINI-SIASA

Rais wa China Xi Jinping kuzuru Korea Kaskazini

Xi Jinping rais wa China (Katikati)
Xi Jinping rais wa China (Katikati) 网络照片
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
Dakika 1

Rais wa China Xi Jinping anatarajiwa kuzuru Korea Kaskazini wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Hii itakuwa ziara ya kwanza ya kiongozi wa China nchini Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 14.

Taarifa kutoka Beijing zinasema kuwa rais Xi, atatembelea Pyongyang siku ya Alhamisi na Ijumaa, baada ya kualikwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Ziara ya kiongozi wa China inakuja wakati huu kuelekea mkutano Mkuu wa G20 nchini Japan, ambapo rais Xi na mwenzake wa Marekani Donald Trump wanatarajiwa kukutana na kuzungumzia masuala ya biashara.

Kim Jong alitembelea China mara nne, kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika harakati za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili lakini pia kutafuta uungwaji mkono ili kuondolewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

Korea Kaskazini inaendelea kuvutana na Marekani kuhusu mradi wake wa nyuklia, huku Washingtin DC ikiendelea kuiwekea vikwazo licha ya kuanza mazungumzo ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.