MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Mkutano wa kihistoria kati ya Trump na Kim wagonga vichwa vya habari

Donald Trump na Kim Jong-un kwenye mpaka wa Korea mbili (DMZ), Panmunjom, Juni 30. 2019.
Donald Trump na Kim Jong-un kwenye mpaka wa Korea mbili (DMZ), Panmunjom, Juni 30. 2019. AFP/Brendan Smialowski

Baada ya mkutano wa Trump na Kim kwenye mpaka wa Korea mbili, maoni mbalimbali yameendelea kutolewa kutoka kona nne za dunia. Baadhi wanaona kwamba mkutano kati ya wawili hao ni "ukurasa wa kihistoria" wakati wengine wanaona tukio hilo kama njia ya mawasiliano.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano kwenye mpaka wa Korea mbili ulikuwa "wa kihistoria", na ni uamuzi wa "kishujaa" wa Donald Trump, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini Korea vimekaribisha, huku vikiendelea kurusha hewani picha ya Kim na Trump wakisabahiana kwa kupeana mkono, mwandishi wa Seoul, Frédéric Ojardias amebaini.

Nchi hizo mbili zimekubaliana kufufua mazungumzo kuhusu nyukilia yaliyokuwa yamesimama.

Mkutano huo umeleta "yasio ya kawaida" kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Pyongyang imeongeza, huku ikihakikisha kuwa maafisa wanaoshiriki mazungumzo kati ya nchi hizo mbili wataanza tena mikutano kujadili makubaliano ya kuangamiza silaha za kemikali, baada ya vikao hivyo kusimama kwa miezi kadhaa.

Akizungumza na wanahabari akiwa pembeni ya Trump, Kim amesema mkutano wao ni ishara ya uhusiano wao ''mzuri sana''.

Akiita urafiki wao ''mzuri'', Trump ambaye awali alimuita Kim ''mtu wa roketi''- amesema ni ''siku nzuri kwa dunia'' na kwamba ''anajivunia kufika kwenye mpaka'' wa nchi hizi za Korea.

Vyombo vya habari vya Korea Kusini pia vimekaribisha mkutano huo, na kusema vina matumaini ya kuanza tena kwa mazungumzo ya nyuklia. "Ukurasa wa kihistoria umeandikwa," gazeti la kila siku la Joongang limeandika, na kukumbusha kwaba "imani kati ya pande mbili inakuja kupitia mawasiliano ya mara kwa mara".