PAPUA NEW GUINEA-USALAMA

Papua New Guinea yakumbwa na mapigano ya kikabila

Waziri Mkuu James Marape ameahidi kutenda haki haraka kwa waathiriwa
Waziri Mkuu James Marape ameahidi kutenda haki haraka kwa waathiriwa GORETHY KENNETH / AFP

Ndani ya kipindi cha siku 3, watu 24 wameuawa nchini Papua New Guinea, ikiwa ni pamoja na watoto na wanawake wajawazito. Vurugu hizi zinatokana na ulipizaji kisasi kati ya makabila mbalimbali katika nchi hii ya Pasifiki. Sababu ya uhasama huu bado hazijajulikana.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya kikabila yameua angalau watu 24, ikiwa ni pamoja na wanawake 16 na watoto walio na umri ulio chini ya miaka 15, katika jimbo la Hela, kanda ya magharibi ya Papua New Guinea. Miongoni mwa waathirika, watoto na wanawake wajawazito waliuawa kwa kupigwa mapanga na risasi, hususan katika kijiji cha Karida. mkuu wa mkoa anasema idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Waziri Mkuu James Marape, ameahidi kutenda haki haraka kwa waathirika. Ametangaza kutuma haraka vikosi vya ziada vya usalama na amewaonya wahalifu wa mauaji kwamba wakati wao "unahesabiwa".

Kwa mujibu wa maafisa katika eneo hilo, machafuko hayo yalifanyika ndani ya kipindi cha siku tatu. Makabila hasimu katika eneo hilo wanakabilina kwa karne kadhaa kwa ajili ya udhibiti wa dhahabu zinazotoroshwa kutoka eneo hilo tajiri katika malighafi. Vurugu huwa zikitokea mara kwa mara, kutokana na udhibiti wa rasilimali lakini pia migogoro ya zamani inayotokana na ubakaji au wizi, au kwa migogoro ya mipaka. Lakini matumizi ya silaha za moto yamesababisha idadi ya vifo kuongezeka. Hili ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo na mamlaka, ambayo ina maafisa wa polisi 40 tu na askari 16 katika eneo lenye wakaazi 400,000, kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, imeshindwa kukabiliana na hali hiyo.