BANGLADESH-NEPAL-MAJANGA ASILI

Mafuriko na maporomoko ya udongo vyaua watu 180 Kusini mwa Asia

Katika eneo la Muzzafarpur, watoto wakijielekeza katika nyumba moja baada ya nyingine, baada ya mafuriko. Eneo la Bihar (kaskazini-mashariki mwa India) ni miongoni mwa  maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo na maporomoko ya udongo.
Katika eneo la Muzzafarpur, watoto wakijielekeza katika nyumba moja baada ya nyingine, baada ya mafuriko. Eneo la Bihar (kaskazini-mashariki mwa India) ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo na maporomoko ya udongo. (Photo : Mouhssine Ennaïmi / RFI)

Mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa vimeua watu wasiopungua 180 kusini mwa Asia, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumanne na mamlaka za nchi zilizoathiriwa.

Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Juni hadi Septemba, ukanda huo ambao ni watano kwa wakaazi wengi duniani, umekuwa ukikumbwa na majanga mbalimbali.

Lakini kila mwaka, mvua pia husababisha vifo na uharibifu mkubwa.

Watoto wasiopungua watano walifariki dunia siku ya Jumatatu nchini Bangladesh, na kukamilisha idadi ya watu 34 ambao wamepoteza maisha katika taifa hilo lenye wakaazi milioni 160.

Watu wengine kumi walifariki dunia katika kambi kubwa za wakimbizi wa Rohingya kusini mashariki mwa Bangladesh, ambako maelfu ya vibanda vimeharibika.

Mafuriko kaskazini mwa nchi pia yameathiri mamia ya maelfu ya watu.

Nchini Nepal, angalau watu 67 walikufa kufuatia mafuriko. Hata hivyo mashahidi wanasema maji yameanza kupungua.