Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki afariki dunia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Yukiya Amano, Vienna, Novemba 22, 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Yukiya Amano, Vienna, Novemba 22, 2018. AFP

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, sekretarieti ya shirika hilo linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa limetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa nchi wanachama, shirika hilo, lenye makaazi yake Vienna, limesema lina "huzuni kubwa", lakini halikutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za kifo chake.

Yukiya Amano, raia wa Japan, ameongoza shirika hilo kwa muda wa miaka 10, akiwajibika hasa kwa kufuatilia ahadio za Iran kwa mkataba wa nyuklia uliofikiwa mnamo mwaka 2015.

Bw Amano amekuwa akikamilisha muhula wake wa tatu, ambao unamalizika Novemba 2021, lakini alikuwa anatarajiwa kutangaza kuachia ngazi mwezi Machi 2020 kwa sababu za kiafya.

Katika barua ambayo alitarajia kutuma kwa wawakilishi wa IAEA ili kutangaza kujiuzulu kwake, Amano alikaribisha "matokeo halisi" yaliyopatikana wakati wa muhula wake "kufikia lengo" atomi kwa amani na maendeleo " , na alisema "amefurahishwa sana kwa mafanikio" ya shirika hilo, kwa ujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la IAEA.

Shirika hilo, lenye makao yake Vienna, linatarajia kumtafuta mrithi wake ambaye atahusika na kufuatilia mpango wa nyuklia wa Iran wakati mvutano unaendelea kuongezeka kati ya Iran na Marekani.