Pata taarifa kuu

Vikosi maalum vyaendesha operesheni ya kumkamata rais wa zamani wa Kyrghyzstan

Almazbek Atambayev mwaka 2017 (picha ya kumbukumbu).
Almazbek Atambayev mwaka 2017 (picha ya kumbukumbu). VYACHESLAV OSELEDKO / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Vikosi maalum nchini Kyrghyzistan vimezindua uperesheni mpya ya kukamata rais wa zamani wa nchi hiyo Almazbek Atambayev. Operesheni ya jana Jumatano imeambulia patupu baada ya askari mmoja kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika kujaribu kumkamata rais huyo wa zamani.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya Wizara ya afya nchini humo afisa mmoja aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wengine 36 walijeruhiwa.

Awali shirika la habari la Interfax lilimnukuu Waziri wa usalama wa ndani nchini humo akisema maafisa wa usalama wanaondoka katika eneo hilo kutokana na utekaji nyara unaofanywa na wafuasi wa Atambayev.

Almazbek Atambayev alishtakiwa mwishoni mwa mwezi Juni kwa ufisadi. Alivuliwa kinga baada ya kutuhumiwa kashfa hiyo.

Almazbek Atambayev alifutilia mbali tuhuma hizo dhidi yake na hadi sasa amekataa kufika mahakamani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.