Pata taarifa kuu
PAKISTANI-INDIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Vikosi vya India vyapiga doria katika maeneo mbalimbali Kashmir

Wanajeshi wa India wakiwa katika kambi yao iliyoshambuliwa na waasi wa wanaotaka kujitenga Panzgam, Kashmir, Aprili 27, 2017.
Wanajeshi wa India wakiwa katika kambi yao iliyoshambuliwa na waasi wa wanaotaka kujitenga Panzgam, Kashmir, Aprili 27, 2017. REUTERS/Danish Ismail

Maafisa wa usalama nchini India, wanapiga doria katika jimbo la Kashmir ambalo kwa muda mrefu limeendelea kuwania na nchi jirani ya Pakistan, wiki hii baada ya India kutangaza kuwa inaliondolea jimbo hilo uhuru wa kujiongoza.

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na wasiwasi wa kutokea kwa makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama, baada ya maombi ya Ijumaa.

Kwa siku tano sasa, mtandao wa Internt umezimwa huku kukiwa na ugumu wa mawasiliano ya simu, suala ambalo limetatiza shughuli za waakazi wa jimbo hilo, wengi wakiamua kusalia nyumbani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress, ametoa wito wa uvumilivu kati ya India na Pakistan kuhusu mzozo huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.