Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Maandamano yaibuka tena kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong

Waandamanaji katika eneo la wageni wanaowasili kwene uwanja wa ndege wa Hong Kong, Agosti 12, 2019.
Waandamanaji katika eneo la wageni wanaowasili kwene uwanja wa ndege wa Hong Kong, Agosti 12, 2019. REUTERS/Thomas Peter
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Hong Kong imeendelea kukumbwa na maandamano makubwa yanayoongozwa na wanaharakati wa naounga mkono demokrasia katika eneo hilo. Shughuli mbalimbali zimezorota katika eneo hilo, baadhi ya maduka, makampuni na shule zimefunga.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong umekumbwa tena Jumanne hii na maandamano makubwa. Waandamanaji wanaounga mkono demokrasia wanaendelea kukabiliana na polisi wa kutuliza ghasia.

Siku ya Jumatatu serikali ya Hong Kong ilichukuwa uamuzi wa kusitisha safari zake za ndege .

Mamlaka ya Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong, ilisitisha safari zake zote kwa siku ya jana wakati waandamanaji wanaoipinga serikali walidhibiti eneo la wageni wanaowasili.

Zaidi ya waandamanaji 5,000 walikusanyika katika eneo la uwanja huo, ambao unatajwa kuwa na pirikapirika nyingi za safari.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, ambae anahusika pia katika mawasiliano ya umma Kong Wing-Cheung alisema taarifa alizonazo ni kwamba sehemu ya wageni wanaowasili kuna zaidi ya waandamanaji 5,000.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.