HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Hong Kong: Viongozi wawili wa maandamano Joshua Wong na Agnes Chow waachiliwa huru

Wanaharakati wawili wanaotetea demokrasia Hong Kong Agnes Chow na Joshua Wong wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari baada ya kukamatwa Ijumaa, Agosti 30, 2019.
Wanaharakati wawili wanaotetea demokrasia Hong Kong Agnes Chow na Joshua Wong wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari baada ya kukamatwa Ijumaa, Agosti 30, 2019. AFP Photos/Lillian SUWANRUMPHA

Saa chache kabla ya maandamano mapya Jumamosi, polisi wa Hong Kong wamekamamata viongozi watatu wa maandamano yanayounga mkono Demokrasia, ikiwa ni pamoja na Joshua Wong na Agnes Chow. Wote wameachiliwa kwa dhamana.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa mwisho wa twitter wa Joshua Wong kabla ya kukamatwa kwake ulikuwa kama wito wa kupinga utawala wa Beijing. Agnès Chow yeye aliandika hivi: "Pigania uhuru, tetea Hong Kong." Wameachiliwa kwadhamana na Joshua Wong tayari ameahidi: ataendeleza vita yake.

Tutaendelea na vita yetu, hata kama watatuzuia, hata kama watatufungulia mashitaka. Tunajua vizuri kuwa polisi ya Hong Jong inaungwa mkono na kutiwa moyo na serikali ya Rais wa China Xi Jingping kutekeleza operesheni hiyo ya kutukamata.

Wananchi wa Hong Kong wanawafahamu viongozi hawa wawili wa maandamano tangu mwaka 2012: wakiwa na miaka 15, wanafunzi hao wawili wa vyuo vikuu waliweza kuhamasisha makumi ya maelfu ya wazazi na wanafunzi dhidi ya kozi mpya ya elimu ya kitaifa.