Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-VIKWAZO-USALAMA

Tehran yaionya Marekani dhidi ya hatua za kijeshi

Rais wa Iran Hassan Rohani na baraza lake la mawaziri, Septemba 18, 2019, Tehran.
Rais wa Iran Hassan Rohani na baraza lake la mawaziri, Septemba 18, 2019, Tehran. Official President website/Handout via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Iran imetupilia mbali madai ya Marekani na Saudi kuhusu kuhusika kwake katika mashambulio ya mitambo ya mafuta ya Saudia. Wakati huo huo Tehran imeonya Marekani dhidi ya shambulio lolote katika ardhi yake.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani uamuzi wa Donald Trump wa kuimarisha zaidi vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, na kuviita vikwazo hivyo "ugaidi wa kiuchumi".

Akiwa ziarani nchini Saudi Arabia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameelezea shambulio la Ijumaa usiku dhidi ya mitambo ya mafuta ya Saudia kama "kitendo cha vita".

Mike Pompeo anaihusisha Iran kwa shambulio hilo. Rais wa Marekani ameagiza kuchukuliwa vikwazo vipya dhidi ya Iran baada ya shambulio dhidi ya mitambo ya mafuta ya Saudi Arabia.

Hata hivyo, Donald Trump, bado ametishia Tehran kukabiliwa na mkono wa chuma. Amesema yuko tayari kwa hatua ya kijeshi. Donald Trump, hata hivyo, amewahi kusema kuwa anapingana na wazo la kuiingiza Marekani katika mzozo mpya.

Katika barua iliyowasilishwa kwa ubalozi wa Uswisi unaowakilisha masilahi ya Marekani nchini Iran, Tehran pia imekanusha kuhusika kwake katika mashambulio ya mitambo ya mafuta nchini Saudi Arabia. Lakini Televisheni ya CBS News ilisema Jumatano kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na Iran na kupitishwa na Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi mkuu wa Iran, akimnukuu afisa wa Marekani ambaye hakutaja jina lake.

Kwa upande wa Robert Miking, mshauri wa zamani wa Barack Obama katika Mashariki ya Kati na kiongozi wa shirika la kimataifa la ICG, inawezekana kabisa kwamba Tehran ndio ilihusika na shambulio hilo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.