JAPAN-NARUHITO-UFALME

Japani: Mfalme Naruhito atangaza kuanza kazi rasmi

Mfalme mpya Naruhito, na Malkia Masako, Mrithi wa Ufalme Akishino na mkewe malkia Kiko wakihudhuria tafrija ya kutawazwa ufalme katika kasri Tokyo, Japan Mei 1, 2019.
Mfalme mpya Naruhito, na Malkia Masako, Mrithi wa Ufalme Akishino na mkewe malkia Kiko wakihudhuria tafrija ya kutawazwa ufalme katika kasri Tokyo, Japan Mei 1, 2019. Kyodo/via Reuters

Mfalme mpya wa Japan Naruhito Jumanne wiki hii ametangaza kutawazwa kwake wakati wa hafla ya kifahari kwenye Kasri ya Mfalme jijini Tokyo mbele ya wageni 2000, ikiwa ni pamoja na wakuu wa nchi na viongozi kutoka nchi takriban 180.

Matangazo ya kibiashara

"Nikilihutubia taifa na dunia, natangaza kutawazwa kwangu," amesema Naruhito,akiambatana na mkewe Masako, ambao wote walikuwa wamevaa vazi la kijadi kwa minajili ya ibada hii ya kipekee.

Naruhito alikua mtawala wa 126 wa Japan Mei 1 baada ya kustaafu baba yake Akihito ambaye alisalia kwenye kiti cha ufalme kwa miaka 30

Mfalme Emeritus Akihito mwenye umri wa miaka zaidi ya 85, mara ya kwanza alitangaza mpango wa kuachia madaraka mwaka 2016, akieleza wasiwasi wake juu ya umri aliofikia na changamoto za kiafya katika kutekeleza majukumu yake.

Mfalme huyo wa Japan aliyeachia madaraka aliingia alichukuwa madaraka mwezi Januari 1989 baada ya kifo cha baba yake, ambaye ni Mfalme wa kipindi cha Vita ya pili ya Dunia Hirohito, ambaye ni wa kwanza kuachia madaraka katika kipindi cha miaka 200.