CHINA-EU-SAKHAROV-HAKI

Ilham Tohti ashinda tuzo ya Sakharov

Ilham Tohti, msomi kutoka Jamii ya Uyghur anayefungwa nchini China.
Ilham Tohti, msomi kutoka Jamii ya Uyghur anayefungwa nchini China. New York Times/ Gilles Sabrie

Bunge la Ulaya limeomba kuachiliwa huru "mara moja" Ilham Tohti, msomi kutoka jamii ya Uyghur ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Xinjiang nchini China. Ilham Tohti ni mwanaharakati anayetetea haki za jamii ya wachache ya Uyghur.

Matangazo ya kibiashara

Leo Alhamisi, 24 Oktoba, mamlaka ya Strasbourg imetoa tuzo ya uhuru wa mawazo ya Sakharov kwa profesa huyo wa zamani wa uchumi katika chuo kikuu cha Beijing, aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kungana na kundi linalotaka "kujitenga" kwa eneo lao.

Hii ni tuzo ya pili ndani ya kipindi cha miezi miwili Ilham Tohti anapata kutoka Ulaya. Tayari Septemba 30, mhadhiri huyo wa zamani wa chuo kikuu cha Beijing alipokea Tuzo la Vaclav-Havel iliyotolewa na Baraza la Ulaya kwa "kutoa nafasi ya kujieleza kwa watu kutoka jamii ya Uyghur". Lakini kwa wakati huu, tuzo hiyo ni ya kifahari zaidi, na haitakosa kukasirisha Beijing.

Kupitia tuzo hii, Ilham Tohti ameandikisha jina lake kwenye kitabu cha historia cha washindi tuzo hiyo kama vle Malala Yousafzai, Kofi Annan, mpinzani wa Wachina Hu Jia, lakini haswa Nelson Mandela, mshindi wa tuzo hiyo mnamo 1988.

Ulimwenguni unatambua kazi kubwa alioifanya Ilham Tohti, mhadhiri wa chuo kikuu cha wachache katika mji wa Beijin, hasa kujitolea kwa kufanya kazi maisha yake yote kwa kuunganisha jamii mbili tofauti kati ya Hans, kabila la walio wengi nchini China (92%), na Uighur, jamii ya Waislamu wachache wanaozungumza lugha ya Kituruki waishio Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China.

Beijing inamshutumu Ilham Tohti kuwa "mwanaharakati anayeunga mkono ugaidi wenye msimamo mkali", ikimaanisha, kutetea uhuru wa Mashariki ya Turkestan, jina lililopewa na wanaharakati wa Uyghur waishio Xinjiang. Mhadhiri huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha maisha mnamo mwaka 2014 katika kesi iliyokosolewa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.

Kabla ya kukamatwa kwake Januari 2014, Ilham Tohti alianzisha tovuti ya UighurOnline, ambayo inashughulikia kwa lugha ya Kichina na Kiuyghur shida za kijamii katika jimbo la Xinjiang.

Tuzo ya Sakharov inayotolewa kutona na michango katika nyanja za haki za binaadamu na uhuru, ilitolewa kwa mara ya kwanza zaidi ya miaka 30 iliyopita. Tuzo hiyo itakabidhiwa kwa mshindi Desemba 18, mjini Strasbourg, Ufaransa.