MAEKANI-IRAN-VIKWAZO

Washington yaweka vikwazo dhidi ya washirika wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa Iran

Waziri wa Fedha wa Marekani Steve Mnuchin (hapa ilikuwa Oktoba 11, 2019).
Waziri wa Fedha wa Marekani Steve Mnuchin (hapa ilikuwa Oktoba 11, 2019). REUTERS/Yuri Gripas

Marekani imeiwekea vikwazo vipya Iran hasa washirika wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo Ali Khamenei. Waziri wa Fedha wa Marekani ametangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran Jumatatu Novemba 4, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya utekaji nyara wa ubalozi wa Marekani Tehran.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi vipya vya Marekani vinalenga maafisa tisa wanaofanya kazi katika ofisi ya Kiongozi Mkuu aw Iran, Ali Khamenei.

Mali za maafisa hao zimezuiliwa nchini Marekani na wamepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote na raia wa Marekani.

Kiongozi Mkuu wa Iran tayari amewkewa vikwazo kama hivyo tangu mwezi Juni mwaka huu. Miongoni mwa maafisa hao waliowekewa vikwazo ni pamoja na mtoto wake, ambaye amemkabidhi majukumu mengi, mkurugenzi katika ofisi yake, mkuu wa mahakama ya Irani na viongozi wengine sita, ambao wote waliteuliwa na Ali Khamenei. "Hatua hizi zinapunguza zaidi uwezo wa Kiongozi Mkuu wa Iran kutekeleza sera yake ya vitisho," Waziri wa Fedha wa Marekani Steve Mnuchin amesema katika taarifa.

"Uamuzi wa kuwateka nyara wanadiplomasia wetu umevunja uhusiano wetu kwa miaka 40, lakini Marekani inajua kuwa wanaoathirika zaidi ni raia wa Iran," Waziri wa Fedha wa Marekani ameongeza. wakati wa hotuba Jumatatu.

Mike Pompeo ametangaza zawadi nono ya dola milioni 20 kwa atakaye toa habari kuhusu hatima ya Robert Levinson, afisa wa zamani wa shirika la Marekani la FBI aliyetoweka nchini Iran mnamo mwaka 2007.