Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Makao makuu ya Chuo Kikuu cha Hong Kong yaendelea kuzingirwa, Beijing yatoa vitisho

Hali ya sintofahamu yaendelea Hong Kong, huku waandamanaji wakiendelea kukabiliana na vikosi vya usalama.
Hali ya sintofahamu yaendelea Hong Kong, huku waandamanaji wakiendelea kukabiliana na vikosi vya usalama. REUTERS/Thomas Peter
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Wanaharakati wa kupigania demokrasia wameanza Jumanne hii asubuhi siku yao ya tatu wakiwa mafichoni katika makao makuu ya Chuo Kikuu cha Hong Kong, baada ya wenzao kuvamiwa usiku.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo China imesema haitofumbia macho hali inayoendelea Hong Kong na kutoa vitisho dhidi ya waandamanaji.

Hata hivyo Rais wa Hong Kong ambaye yuko chini ya mamlaka ya China, Carrie Lam, amewataka waandamanaji waliokimbilia katika Chuo Kikuu cha Hong Kong kuweza kujisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya hatua kali hazijachukuliwa.

Maandamano yaliendelea Jumatatu wiki hii, na makabiliano makali yalishuhudiwa baina ya polisi na wanaharakati wa kupigania demokrasia walioingia ndani ya majengo ya chuo kikuu, na kuwashambulia polisi kwa fataki na mishale. Polisi walitishia kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji hao, ikiwa hawangeacha kuwalenga maafisa wake.

Miale ya moto iliyotokana na mfululizo wa milipuko ilionekana kutoka ndani ya majengo pindi maafisa wa polisi wa kutuliza fujo walipoingia kwenye viunga vya chuo hicho mapema Jumatatu alfajiri.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.