BURMA-GAMBIA-ICJ-HAKI

Rohingyas: Aung San Suu Kyi kutetea Burma mbele ya Umoja wa Mataifa

Aung San Suu Kyi, kiongozi wa zamani wa upinzani na mkereketwa wa kidemokrasia nchini Burma.
Aung San Suu Kyi, kiongozi wa zamani wa upinzani na mkereketwa wa kidemokrasia nchini Burma. REUTERS/Athit Perawongmetha

Kiongozi wa zamani wa upinzani na mkereketwa wa kidemokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi, ataongoza ujumbe wa serikali mbele ya mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa kwa kutetea nchi yake, serikali ya Burma imebaini.

Matangazo ya kibiashara

Burma inakabiliwa na shinikizo la kisheria kuhusu hatima ya Waislamu kutoka jamii ya walio wachache ya Rohingya.

Hivi karibuni Gambia, iliyowakilisha nchi 57 wanachama wa jumuiya ya ushirikiano wa Kiislamu, iliwasilisha mashtaka dhidi ya Burma kwa "vitendo vya mauaji ya halaiki" mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Mwezi Agosti 2017, Waislamu zaidi ya 740,000 kutoka jamii ya walio wachache ya Rohingya walitoroka Myanmar, yenye wakaazi wengi kutoka jamii ya Wabudhi, baada ya jeshi kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi mashambulizi ya waasi kutoka jamii ya Rohingya karibu na mpaka wa Burma.

Baada ya kuteshwa na kufanyiwa ukatili na wanajeshi wa Burma na wanamgambo wa Kibudhi, watu kutoka jamii ya Rohingya walilazimika kukimbilia katika kambi nchini Bangladesh.

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa (ICJ), yenye makao yake makuu mjini Hague, inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi hiyo mnamo mwezi Desemba.

Aung San Suu Kyi, mkuu wa serikali ya Burma, ataongoza ujumbe wa serikali ili"kutetea masilahi ya kitaifa ya Burma," Ofisi yake imesema, huku ikibani kwamba mawakili mashuhuri wa kimataifa pia wamemesajiliwa.

Burma imetupilia mbali tuhuma za kuangamiza kabila au mauaji ya kimbari, na imesema imeunda kamati za kuchunguza madai hayo ya mauaji.

Gambia sio pekee yakea mabyo imeanzisha mpango huo dhidi ya Burma.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), pia yenye makao yake makuu mjini Hague, wiki iliyopita ilitoa idhni kwa uchunguzi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya watu kutoka jamii ya Rohingya.