Pata taarifa kuu
HONG KONG-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Carrie Lam: Wapiga kura wameonyesha kutoridhishwa na uongozi wa mji wa Hong Kong

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa Halmashauri za mitaa Novemba 24, 2019.
Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa Halmashauri za mitaa Novemba 24, 2019. REUTERS/Thomas Peter
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Kiongozi wa Jimbo la Hong Kong Carrie Lam amekiri kuwa kiwango kikubwa cha ushiriki katika uchaguzi wa Halmashauri za mitaa uliofanyika Jumapili, umeonyesha kuwa wapiga kura wametaka mabadiliko.

Matangazo ya kibiashara

Carrie Lam amebaini kwamba ushindi wa kambi inayounga mkono demokrasia unaashiria kuwa wananchi wameonyesha kutoridhishwa na uongozi wa mji huo, ambao umeendelea kukumbwa na maandamano makubwa kwa miezi kadhaa.

Kambi ya wanaounga mkono demokrasia imepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi huo wa Hamashauri za mitaa. Kambi ya wanaounga mkono demokrasia imepata karibu asilimia 90 ya viti 452 kwenye Baraza la madiwani, tofauti na miaka minne iliyopita ambapo kambi hiyo ilipata viti 100.

Kulingana na takwimu rasmi, kiwango cha ushiriki kilikuwa karibu mara mbili ikilinganishwa na mwaka 2015 kwa zaidi 71% katika mji wenye wakaazi milioni 7.4.

Katika taarifa yake, Lam amesema kwamba kura inaakisi kutoridhika kwa wananchi na hali ilivyo kwa sasa. Ameongeza kwamba serikali itasikiliza kwa unyenyekevu na kutafakari sana juu ya uchaguzi ambao vyama vinavyounga mkono demokrasia vimeshinda kwa wingi katika halmashauri za wilaya zote 18 za jiji hilo na kuwapokonya viti wagombea walizoeleka wa upande unaounga mkono serikali ya China.

Ingawa halmashauri za wilaya zinahusika zaidi na masuala ya kijamii, ni miongoni mwa wawakilishi wa kundi la wateule 1,200 watakaomteua kiongozi ajae wa mji huo mwaka 2022.

Hata hivyo katika mkutano na waandishi wa habari nchini Japan, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema Hong Kong bado ni sehemu ya China, bila ya kujali kinachotokea katika eneo hilo lenye mamlaka yake ya ndani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.