KOREA KASKAZINI-MAREKANI- KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Washington yajaribu kufufua mazungumzo na Pyongyang

Mjumbe wa Marekani katika mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, Stephen Biegun, yuko ziarani Seoul, nchini Korea Kusini tangu Jumapili Desemba 15.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kushoto) akimkaribisha mjumbe wa Marekani katika mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambaye amewasili Seoul kujaribu kufufua mazungumzo kati ya Washington na Korea Kaskazini.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kushoto) akimkaribisha mjumbe wa Marekani katika mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambaye amewasili Seoul kujaribu kufufua mazungumzo kati ya Washington na Korea Kaskazini. YONHAP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya siku tatu, lengo lake ni kujaribu kufufua mchakato wa mazungumzo na Korea Kaskazini.

Ziara hii inakuja wakati serikali ya Korea Kaskazini inaanza tena majaribio yake ya makombora, na inatishia Marekani kuanza tena uchochezi mwishoni mwa mwaka huu. "Ni wakati wa kufanya kazi (...) mnajua jinsi ya kutupata," amesema Stephen Biegun alipowaili nchini Korea Kusini.

Korea Kaskazini inataka ipunguziwe mzigo wa vikwazo ilivyowekewa.

Mwaliko huu umewasilishwa kwa Pyongyang, na hali hiyo inaonyesha kwamba hakuna mkutano uliopangwa mpakani kati ya mjumbe wa Marekani na wajumbe wa Korea Kaskazini katika mazungumzo. Stephen Biegun anafanya ziara nchini Korea Kusini wakati Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake la pili la makombora siku ya Ijumaa baada ya jaribio lingine kufanyika siku sita zilizopita.

Korea KAskazini inaonyesha kwamba iko karibu kuanza tena hadharani mpango wake wa nyuklia na wamajaribio ya makombora ya masafa marefu na Kamati Kuu ya Chama tawala nchini humo inataraji kukutana hivi karibuni kuhalalisha kurejea kwa hali nzito.

Lakini Mrekani imesema haifikirii kupunguza vikwazo dhidi ya Pyongyang.

Rais wa Marekani Donald Trump amekataa kuondoa vikwazo hadi pale Korea Kaskazini itakapoacha mpango wake wa Nyuklia.