KAZAKHSTAN-USALAMA-AJALI

Watu 14 wafariki dunia katika ajali ya ndege Kazakhstan

Almaty, mji mkuu wa Kazakhstan. Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imeongeza kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Bek Air ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.
Almaty, mji mkuu wa Kazakhstan. Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imeongeza kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Bek Air ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili. wikipedia

Ndege iliyokuwa ikisafiri na watu 100 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Almaty, nchini Kazakhstan, na kuua watu wasiopungua 14, viongozi katika nchi hiyo ya Asia ya Kati wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imesema kwamba kulikuwa na abiria 95 na wafanyakazi watano ndani ya ndege hiyo.

'Majeruhi 17 wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya sana, watu 14 wamekufa papo hapo,' mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty, jiji kuu la nchi hiyo, imebaini katika ujumbe uliotumwa kupitia ujumbe wa Telegramu.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Almaty imeongeza kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Bek Air ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.

Katika ujumbe wa rambirambi kwenye twitter, Rais Kassym-Jomart Tokayev pia amehakikisha kuwa 'maafisa wawili wataadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria'.

Ajali hiyo ilitokea karibu na Kzyl-tu, mji unaopatikana Kaskazini mashariki mwa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa zamani wa Kazakhstan.