Pata taarifa kuu
UKRAINE-USALAMA-SIASA

Serikali ya Ukraine na waasi wabadilishana wafungwa

Rais Volodymyr Zelenskiy akisalimiana na mfungwa aliyeachiliwa huru wakati wa kuwasili kwake Kiev, Desemba 29, 2019.
Rais Volodymyr Zelenskiy akisalimiana na mfungwa aliyeachiliwa huru wakati wa kuwasili kwake Kiev, Desemba 29, 2019. Ukrainian Presidential Press Service/Handout via REUTERS

Serikali ya Ukraine na waasi wa Mashariki mwa nchi hiyo wanaoungwa mkono na Urusi wamebadilishana wafungwa takribani 200. Zoezi hilo ambalo linapingwa na baadhi linalenga kupunguza uhasama na Urusi katika mgogoro huo wa kijeshi unaoendelea mpaka sasa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

'Ni vizuri sana, nimefurahi,' amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye amekuwa akitaka zoezi hilo lifanyike, ikiwa ni zoezi la kwanza la aina yake tangu mwaka 2017, kabla ya sikuu Kuu ya Mwaka Mpya, na kukaribisha wenanchi wenzake kwenye uwanja wa ndege wa Kiev.

Wakati huo huo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamepongeza hatua iliyofikiwa kati ya serikali ya Kiev na waasi wa Mashariki.

Zoezi hili la kubadilishana wafungwa 'lingelishindwa kwa muda wowote, wakati inafahamika kwamba raia wengi wa Ukraine wanaendelea kuzuiliwa nchini Urusi na Crimea, rasi ya Ukraine iliyounganishwa na Urusi mnamo mwaka 2014, ' amesema rais wa Ukraine.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza mjini Paris mnamo Desemba 9. Viongozi hao walikubaliana kuchukua hatua za kusitisha vitaa pekee vinavyoendelea barani Ulaya kwa sasa.

Mahusiano kati ya Ukraine na Urusi yaliharibika tangu 2014, Urusi ilipoinyakuwa rasi ya Crimea na kuwasadia waasi wa mashariki mwa Ukraine kuanzisha vuguvugu la kutaka kujitenga.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.