UKRAINE-URUSI-AJALI

Kesi kuhusu ajali ya ndege MH17 yaanza nchini Uholanzi

Kesi ya kwanza kuhusu ajali ya ndege MH17 inafunguliwa Jumatatu nchini Uholanzi, licha ya wanaume wanne wanaoshukiwa kuwa walisababisha mlipuko wa ndege hiyo katika anga la Ukraine, miaka mitano zaidi iliyopita kutofika mahakamani.

Picha ya mabaki ya Boeing 777, ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines wakati wa kuwasilisha ripoti ya mwisho kuhusu sababu za ajali ya ndege hiyo MH17, Oktoba 13, 2015 huko Gilze Rijen, Uholanzi
Picha ya mabaki ya Boeing 777, ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines wakati wa kuwasilisha ripoti ya mwisho kuhusu sababu za ajali ya ndege hiyo MH17, Oktoba 13, 2015 huko Gilze Rijen, Uholanzi © AFP
Matangazo ya kibiashara

Boeing 777 ya Shirika la ndege la Malaysia, iliyokuwa ikitokea Amsterdam kwenda Kuala Lumpur Julai 17, 2014, ilipigwa kombora aina ya BUK lililotengenezwa Urusi ikiwa hewani juu ya eneo la kivita wakati wa mapigano kati ya vikosi vya Ukraine na wapiganaji walioungwa mkono na Urusi katika eneo la Mashariki mwa Ukraine.

Watu 298 walio wakidafiri na dege hiyo, ikiwa ni pamoja na raia 196 kutoka Uholanzi, waliuawa.

Raia watatu kutoka Urusi (Sergei Dubinsky, Igor Guirkine na Oleg Poulatov), pamoja na raia mmoja wa Ukraine (Leonid Khartchenko), wanashtumiwa kuua na kusababisha ajali hiyo.

Washukiwa wa kwanza kushtakiwa katika kesi hii, wanatuhumiwa na ofisi ya mashtaka ya Uholanzi kusafirisha mfumo wa kombora la kulipua ndege aina ya BUK, kabla ya kurushwa na watu wengine wasiojulikana.