URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Urusi yathibitisha visa zaidi ya 24,000 vya maambukizi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema amesema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuwa kuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi..
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema amesema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuwa kuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi.. Sputnik/Aleksey Nikolskyi/Kremlin via REUTERS

Mamlaka ya Urusi inayohusika na janga la Covid-19 kutokana na ugonjwa huo imetangaza visa vipya 3,388, na kufanya idadi ya visa vya maambukizi kufikia 24,490, na kusababisha vifo vipya 28 kwa jumla ya vifo 198.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya.

"Tunaona kuwa hali inabadilika kila siku na kwa bahati mbaya inazidi kuwa mbaya. Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka, haswa idadi ya wale walio na hali mbaya inazidi" alisema.

Putin, ambaye alifanya tathmini juu ya coronavirus katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika kwa njia ya video, amesema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuwa kuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi.

Rais Vladimir Putin alibaini kuwa, ikiwezekana, vifaa vya jeshi pia vinaweza kutumiwa kupambana na janga hilo, ambalo Umoja wa Mataifa ulisema linatishia ulimwengu.