URUSI-CORONA-AFYA

Visa vipya karibu 6,000 vya maambukizi vyaripotiwa nchini Urusi

Hospitali mpya iliyojengwa kwa kuwapokea wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona nje kidogo ya mji wa Moscow.
Hospitali mpya iliyojengwa kwa kuwapokea wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona nje kidogo ya mji wa Moscow. Denis Voronin/Moscow News Agency/REUTERS

Idadi ya watu walioambukizwa rasmi virusi vya Corona nchini Urusi imefikia 68,622, baada ya kuripotiwa visa vipya 5,849 vya virusi hivyo, ikilinganishwa na Alhamisi, mamlaka ya afya nchini Urusi imebaini.

Matangazo ya kibiashara

Watu watu sitini zaidi wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19, na kufikisha idadi ya vifo vilivyothibitishwa 615, mamlaka hiyo imeongeza.

Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya.

"Tunaona kuwa hali inabadilika kila siku na kwa bahati mbaya inazidi kuwa mbaya. Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka, haswa idadi ya wale walio na hali mbaya inazidi" alisema.

Putin, ambaye hivi karibuni alifanya tathmini juu ya ugonjwa wa Covid-19 katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika kwa njia ya video, alisema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuwa kuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi.

Rais Vladimir Putin alibaini kuwa, ikiwezekana, vifaa vya jeshi pia vinaweza kutumiwa kupambana na janga hilo, ambalo Umoja wa Mataifa ulisema linatishia ulimwengu.