JAPANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Japani kuongeza muda wa dharura hadi Mei 31

Serikali ya Japani inatarajiwa kutangaza hatua mpya za kuzuia kudhibiti janga hilo nchini Japan ambapo karibu watu 15,000 wameambukizwa na watu zaidi ya 500 wamefariki dunia kutokana na Covid-19.
Serikali ya Japani inatarajiwa kutangaza hatua mpya za kuzuia kudhibiti janga hilo nchini Japan ambapo karibu watu 15,000 wameambukizwa na watu zaidi ya 500 wamefariki dunia kutokana na Covid-19. Reuters / Toru Hanai

Serikali ya Japani inapanga kuongeza muda wa hali ya dharura iliyotangawa kwa minajili ya kupambana na janga la Corona hadi Mei 31, Waziri wa Uchumi Yasutoshi Nishimura amesema katika taarifa Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Muda wa hali ya dharura kawaida ungelimalizuika Jumatano wiki hii, siku ya mwisho ya wiki moja iliyotangazwa na serikali kwa kuthibiti janga la Corona.

Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe anatarajiwa kulihutubia taifa leo Jumatatu.

Serikali pia inatarajiwa kutangaza hatua mpya za kuzuia kudhibiti janga hilo nchini Japan ambapo karibu watu 15,000 wameambukizwa na watu zaidi ya 500 wamefariki dunia kutokana na Covid-19.

Wakati huo huo, serikali inaweza kulegeza hatua kadhaa za watu kutotembea, hasa kuruhusu kufunguliwa tena kwa maeneo ya biashara, hata katika mikoa iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo.

Hali ya dharura nchini Japan inawapa magavana wa mikoa uwezo wa kuweka masharti ya watu kutotembea na kufungwa kwa biashara.