CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kesi mpya tatu za maambukizi zathibishwa China

Ugonjwa wa Covid-19 ulianzia katikati mwa China, katika jiji la Wuhan mwezi Desemba mwaka jana.
Ugonjwa wa Covid-19 ulianzia katikati mwa China, katika jiji la Wuhan mwezi Desemba mwaka jana. STR / AFP

Maafisa wa afya Nchini China wamebaini leo Jumatatu kuwa watu watatu wamepatikana na virusi vya Corona katika China Bara. Pia wamebaini kwamba hakuna kifo chochote kinachohusiana na ugonjwa huo ambacho kimeripotiwa.

Matangazo ya kibiashara

China imeendelea kunyooshewa kidole cha lawama na Marekani kwamba ilipuuzia hatari ya ugonjwa wa Covid-19 na kusababisha nchi nyingi kuathirika na ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Covid-19 ulianzia katikati mwa China, katika jiji la Wuhan mwezi Desemba mwaka jana.

Tume ya Kitaifa ya Afya imebaini katika mkutano wake wa kila siku kwamba watu wote watatu walioambukizwa virusi hivyo ni raia kutoka nchi za kigeni.

Kwa jumla, kulingana na takwimu za tume hiyo, watu 82,880 wameambukizwa virusi vya Corona katika China Bara na kusababisha vifo vya watu 4,633.Zaidi ya watu milioni 3.5 waambukizwa virusi vya Corona duniani