URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Urusi yathibitisha visa vipya zaidi ya 10,500 vya maambukizi

Mamlaka ya afya nchini Urusi pia imeripoti vifo vipya 86 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umewauwa watu 1,537 nchini humo.
Mamlaka ya afya nchini Urusi pia imeripoti vifo vipya 86 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umewauwa watu 1,537 nchini humo. Sofya Sandurskaya/Moscow News Agency/Handout via REUTERS

Nchi ya Urusi inaendelea kukabiliwa ugonjwa wa Covid-19. Idadi ya visa vya maambukizi inaendelea kuongezeka nchini humo siku baada ya siku. Zaidi ya visa zaidi ya 10,500 vya maambukizi vimethibitishwa ndani ya saa 24.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Urusi imefikia 165,929, mamlaka nchini humo imetangaza.

Kwa maambukizi ya watu 10,559, idadi inayoongezeka kila siku, visa vya maambukizi vilivyothibitishwa vinazidi kiwango cha watu 10,000 kwa siku ya nne mfululizo.

Mamlaka ya afya ya Urusi pia imeripoti vifo vipya 86 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umewauwa watu 1,537 nchini humo.

Marufuku ya watu kubaki nyumbani inaendelea kutekelezwa katika majimbo mbalimbali ya Urusi, huku serikali ikiwataka raia kuheshimu hatua zilizowekwa kama mapambano dhidi ya janga hatari ya Covid-19.