URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 11,000 za maambukizi zathibitishwa nchini Urusi

Maafisa wa Urusi na wafanyakazi wa afya wakivaa mavazi ya kujikinga na maambukizi ya Corona wakikaguwa abiria kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo hko Mosow, Urusi, Machi 7, 2020.
Maafisa wa Urusi na wafanyakazi wa afya wakivaa mavazi ya kujikinga na maambukizi ya Corona wakikaguwa abiria kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo hko Mosow, Urusi, Machi 7, 2020. REUTERS/Stringer

Urusi imetangaza leo Alhamisi visa vipya 11,231 vya maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya saa 24 zilizopita, ongezeko la maambukizi kwa kila siku ambayo yamefanya kufikia idadi ya maambukizi 177,160 nchini kote tangu kuzuka kwa ugonjwa huo nchini Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Urusi imethibitisha wakati huo huo vifo vipya 88 vilivyotokana na ugonjwa huu ambao watu wengine waliambukizwa na kusababisha vifo jumya ya watu 1,625 nchini Urusi.

Huko Moscow, eneo lililoathiriwa zaidi, ngezeko la maambukizi kwa kila siku pia yamefikia rekodi ya kesi mpya 6,703 za maambukizi zilizothibitishwa ndani ya saa 24.

Jumatano wiki hii Meya wa Moscow Sergei Sobyanin, alisema kwamba idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi zimeongezeka katika mji mkuu kutokana na kuongeza kasi kwa zoezi la vipimo.